Vikosi vya majeshi ya Uganda vimeondoka kwenye makazi ya kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu ‘Bobi Wine’ baada ya Mahakama nchini humo kuamuru kufanya hivyo siku tatu zilizopita.
Majeshi hayo yalikua yamezingira nyumba ya ‘Bob Wine’ na kumuweka kizuizini tangu Januari 14,2020.
Vikosi hivyo vya usalama viliweka kambi nyumbani kwa Bobi ‘Wine’ mara baada ya uchaguzi kwa kile walichodai kuwa ni kumlinda.
Uchaguzi huo mkuu wa Uganda, ulimpa ushindi Rais Yoweri Museveni, matokeo ambayo yamepingwa na ‘Bob Wine’ akidai kuwa uligubikwa na udanganyifu.