Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) imetaja makundi yaliyo hatarini kupata Virusi vya UKIMWI ambayo ni pamoja na wanaofanya ngono kinyume na maumbile, wanaotumia Dawa za Kulevya na wale wanaofanya biashara ya ngono.
Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko amesema UKIMWI bado ni tatizo kubwa kijamii na kiuchumi kwa Watanzania, kutokana na kuendelea kuwepo kwa maambukizi mengi hasa kwa makundi hatarishi.
Ameyataja makundi mengine kuwa ni madereva wa malori yaendayo masafa marefu, wafanyakazi wa kwenye mashamba makubwa, Wavuvi na wanaofanya kazi Migodini.
Takwimu zinaonesha kundi la Vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 ndiyo limeathirika zaidi hususan Vijana wa kike.