“Wakati umefika wa kuanza kuweka mikakati ya lugha ya Kiswahili kutumika katika masuala ya Kimahakama na Kisheria katika ngazi zote, Kiswahili kinatumika AU, SADC, EAC, sioni sababu ya kwanini Mahakama hamtumii Kiswahili” JPM
“Jaji Mkuu hapa umezungumza Kiswahili kizuri kuliko changu cha Kisukuma, lakini ukienda kuhukumu unaandika Kiingereza, hicho Kiswahili kimepotelea wapi, hii ni changamoto kubwa, lazima tubadilike na tukipende kilicho chetu” JPM
“Ukimuandikia hukumu Mtu kule Kijijini, Biharamulo, hukumu imeandikwa kwa Kiingereza yule Bibi Kizee wa Kijijini aende akatafute wa kutafsiri, tunatengeneza kero kwa Wananchi, kuandika hukumu kwa Kiswahili sio dhambi.” Rais Dk. John Pombe Magufuli