Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) Dkt. Yusuph Ngenya amezindua mafunzo ya siku tano ya uandaaji wa viwango shirikishi iliyoshirikisha wazalishaji wa bidhaa mabalimbali.
Mkurugenzi mkuu wa TBS Dkt. Ngenya amezindua mafunzo hayo Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro yaliyoandaliwa na TBS, EAC na GAZ ikihusisha wazalishaji wa bidhaa mabalimbali za viungo, chai na kahawa.
Dkt Ngenya amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaandaa wadau wa sekta mbalimbali kuweka viwango vinavyofaa ili utekelezaji wake uwe rahisi.
Amesema kulikuwa na changamoto ya wadau kutotambua majukumu yao katika kutengeneza viwango shirikishi hivyo kupitia mafunzo hayo wafahamu wajibu wao mkubwa juu ya viwango.
“Bidhaa nyingi zaidi ya 2,000 hivi sasa zina viwango hivyo waandaji wafike TBS ili kupata alama ya ubora na bidhaa zao zinapata nafasi ya kutumika kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki,” Dkt. Ngenya
Ofisa Mkuu wa viwango kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki, Stella Apolot amesema kupitia mafunzo hayo yaliyoandaliwa kupitia EAC, GAZ na TBS wadau watatambua namna ya kufanya katika kuandaa bidhaa bora zaidi ya viwango.
Amesema wadau hao wanapaswa kutambua kuwa utekelezaji wa viwango unapaswa kuwa rahisi kwa walaji na wasiwe watumiaji pekee.
Mwenyekiti wa kamati ya viwango wa TBS wa chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM, Dk Stephen Nyandoro amesema anatarajia washiriki watajifunza kuandaa na kuoanisha viwango mabalimbali katika nchi za Afrika Mashariki.
“Nchi nyingine za Afrika Mashariki hazipo vizuri kwenye biashara ya viungo ila kuna wenzetu wametoka Zanzibar wamebobea kwenye viungo na biashara ya viungo na baadhi ya maeneo ya Tanzania Bara,” Dk Nyandoro.
Mshiriki kutoka Zanzibar Khamis Issa Mohamed ambaye anasafirisha bidhaa za viungo kutoka Zanzibar kwenda Ulaya amesema utaratibu wa kuoanisha viwango ndani ya nchi za Afrika Mashariki utaongeza tija kwenye bidhaa zao.
Mohamed amesema baada ya mafunzo hayo watajenga uelewa mzuri zaidi na kuwekwa utaratibu wa viwango vinavyolingana.
“Unapokuwa unasafirisha bidhaa inapaswa kuwa na viwango vinavyotakiwa na kuwa balozi kwani unapofanya vizuri unaitangaza nchi ila ukipeleka bidhaa isiyo na viwango unaitukanisha nchi yako.