Rais wa Marekani, Joe Biden ametishia kuirejeshea Myanmar vikwazo baada ya Jeshi la Nchi hiyo kuchukua madaraka, huku likikataa kukubali matokeo ya Uchaguzi uliofanyika Novemba 2020.
Biden amesema nguvu haipaswi kupindua matakwa ya wananchi au kujaribu kufuta matokeo ya Uchaguzi wa Kidemokrasia. Amesisitiza Marekani itasimamia Demokrasia pale inapohatarishwa.
Chama cha Kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi, ambaye anashikiliwa pamoja na Maafisa wengine kinashutumiwa kwa udanganyifu kufuatia ushindi wake katika Uchaguzi.
Jeshi tayari limebadili Mawaziri na Manaibu 11 wakiwemo wa Fedha, Afya pamoja na Mambo ya Nje na Ndani. Umoja wa Mataifa (UN), Uingereza, Umoja wa Ulaya (EU) pia wamekemea kinachoendelea, na kuna hofu ya maandamano na vurugu.
“TUNAIBIANA DAWA HAKI YA MUNGU TUTAMFUNGA KILA MTU, NILETE USHAHIDI?” MOLLEL AJIBIWA USILETE