Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa wapo katika mchakato wa kufungua kituo cha huduma kwa wateja ‘Customer Service Center’ kitakachowasaidia wakulima kuwasilisha changamoto zao mbalimbali.
Bashe amebainisha hayo leo bungeni Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu “Tupo katika hatua za mwisho kuanzisha kitu kinaitwa ‘Customer Service Center’ ambapo mkulima popote alipo nchini ataweza kupiga simu bure pale atakapopata pembejeo feki au kupata tatizo la kiatilifu au ugonjwa katika Wilaya yake ili aweze kuhudumiwa kwa wakati” Bashe.
Bashe amewahimiza wakulima pindi wanapoenda kununua pembejeo kuhakikisha wanapata risiti ya EFD ya muuzaji ili atakapopatwa na tatizo Serikali iweze kumchukulia hatua muhusika.