Baada ya kuwepo mjadala mtandaoni kuhusu kumpa hela (matunzo) mwanamke unaekuwa nae kwenye mahusiano, ambapo wapo wanaodai sio lazima kumpa mwanamke hela huku wengine wakisema ni wajibu wa lazima mwanaume kumpa mwanamke wake hela. Swala limemfikia Mwijaku na hapa amefunguka ishu hiyo.
‘Vitabu vya Mungu vinasema Mwanamke atazaa kwa uchungu na Mwanaume utatafuta kwa Jasho hiyo ni hekima sana, Kwahiyo Mwanamke ana haki ya kupewa kwani Mwanaume ni kiongozi wa familia’- Mwijaku
‘Mwanamke akitoa pesa kwenye familia labda kwa mapenzi yake na sio kumpangia na naomba watu wajue kingine Mwanamke ni pambo kwetu sisi Wanaume ndio maana mitandaoni wanawake wengi wamekasirika kauli ya kutopewa hela ila wana haki ya kupewa hela’- Mwijaku
MWIJAKU AJITAMBA “MWANAMKE WANGU HAWEZI KUNIACHA, KILA MWEZI NAMPA MILIONI YA KUSUKA/NAHONGA VIZURI”