Wanafunzi zaidi ya 2500 wa Shule ya Msingi King’ongo Kata ya Saranga wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam, wameondokana na adha ya kukaa chini kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa kufuatia baadhi ya madarasa mapya kukamilika.
Vyumba hivyo vya madarasa zaidi ya tisa vimejengwa huku vingine vikiendelea na hatua za uwekaji sakafu ambapo ujenzi huo umetumia takribani wiki tatu kufuatia agizo la Rais Dk .John Pombe Magufuli.
AyoTV imefika shuleni hapo nakushuhudia wanafunzi wakiwa wanatumia baadhi ya madarasa mapya pamoja na madawati jambo ambalo limewafanya kuepukana na changamoto ya kukaa chini iliyokuwa inawakabili kwa muda mrefu.