Tanzania kwa mara ya kwanza katika historia March 18 na 19 2021 itaandika historia kwa kufanya mkutano mkubwa wa soka (Tanzania Football Summit) ambao utawakutanisha wadau mbalimbali wa soka Ulimwenguni.
Mkutano huo mkubwa soka umeandaliwa na AfriSoccer kwa maslahi mapana ya kuhakikisha wadau wa soka Tanzania kuanzia makocha, wachezaji, mawakala, viongozi wa soka na watu mbalimbali wanaojihusisha na mchezo wa soka kwa namna moja au nyingine.
CEO wa AfriSoccer Peter Simon akiwa kaambatana na Mkuu wa idara ya habari na masoko TFF Boniface Wambura, Muwakilishi wa LaLiga Tanzania na Rwanda Alvaro Paya pamoja na muwakilishi kutoka Serikalini kupitia Wizara ya Michezo wameweka wazi faida za mkutano huo na mada zitakazotolewa.
”Tumekuja na hii Tanzania Football Summit ambao ni mkutanomkubwa wa mpira wa miguu Tanzania, mkutano huu unafanyika kwa mara ya kwanza Tanzania kwa ukubwa wake ambao utakutanisha wadau mbalimbali wa mpira wa mguu wa ndani na nje ya nchi”>>> Peter Simon
Baadhi ya watu watakaokuwepo ni mchezaji wa zamani wa Senegal Kalilou Fadiger, Mtaalam wa Masoko Kelvin Twissa, Rais wa TFF Wallace Karia, Eng Hersi Said kutoka Yanga, Mr Senzo Mbatha na Mtendaji Mkuu wa LaLiga nchini Afrika Kusini.