Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Lindi, imemuhukumu mkazi wa Kata ya RahaLeo, Ustaadhi Selemani Ally (58) kutumikia kifungo cha miaka (20) baada ya kupatikana na hatia ya udhalilishaji wa kingono kwa mtoto mwenye umri wa miaka {12}, jina limehifadhiwa.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo,Muyongwa Magala baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Mashtaka.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mshtakiwa aliulizwa kama anazo sababu zitakazoishawishi mahakama isimpe adhabu kali kwa kosa linalomkabili, ambapo aliiomba Mahakama asipewe adhabu kali na hatarudia tena kutenda kosa la aina hiyo.
Baada ya utetezi huo, Hakimu Magala alimuuliza Wakili wa Serikali, Yahaya Gumbo kama anazo kumbukumbu kwa makosa ya zamani na kujibu hana, lakini akaiomba mahakama kumpa mshtakiwa adhabu kali ili kukomesha vitendo vya udhalilishaji.
Hakimu Magala akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 88/2020, kupitia kifungu 138 C (1) (a) (b) cha sheria kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la 2019, akamhukumu mwalimu huyo wa madrasa, Selemani Ally kutumikia kifungo cha miaka 20 jela na atakapomaliza amlipe mlalamikaji fidia ya Sh,600,000/-.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa Serikali Gumbo, kuwa mshitakiwa ni mwalimu wa madrasa na amekabidhiwa watoto kuwafundisha elimu ya dini lakini amekiuka maadili na kumdhalilisha kingono mtoto huyo mwenye umri wa miaka (12).
Gumbo alidai kuwa mshitakiwa licha ya kuwa na umri mkubwa na mwalimu wa dini, amekuwa na tabia ya kumtomasa maziwa mtoto huyo na baadae akalalamika kwa kutoa taarifa kwa wazazi wake, ambao nao walichukua hatua ya kulifikisha suala hilo Polisi, ambao walimfikisha mahakamani.
EXCLUSIVE: MAAJABU YA MTOTO GENIUS WA HESABU, “SIJAFUNDISHWA, WAKUBWA HAWANIWEZI”