Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, imepigiwa kura na kushinda kuwa mbuga bora zaidi ya hifadhi ya wanyama duniani.
Hayo yamesema mapema leo Machi 3, 2021 mjini Morogoro na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbalo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanayamapori duniani yaliyokwenda sambamba na mkutano wa wadau wa sekta ya utalii.
Akizungumza katika hafla hiyo Dk. Ndumbalo alisema Tanzania imeshinda tuzo hiyo na kuwa ya kwanza kupitia hifadhi ya Taifa ya Serengeti, huku Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Mlima Kilimanjaro zikiwa zimeshika nafasi za juu katika tuzo hizo ambazo hutolewa na Chief Traveler Award (CTA).
“Yalichaguliwa maeneo 25 yanayovutia zaidi kwa utalii kote duniani, katika hayo maeneo matatu yametoka Tanzania, ambapo eneo la kwanza lililopigiwa kura na kushinda kwa kuwa kivutio bora zaidi duniani ni, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, huku hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Tarangire zikiwa ni miongozi mwa maeneo bora zaidi ya utalii,” Dk. Ndumbalo.