Rais wa Zanzibar Dkt. Mwinyi amemuapisha Dkt.Saada Mkuya Salum kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu kwa Kwanza wa Rais, pia amemuapisha Omar Said Shaaban kuwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda na amemuapisha pia Nassor Mazrui kuwa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.
Hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika leo katika ukumbi wa Ikulu, Zanzibar.