Waziri wa Ardhi, Nyumbani na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametangaza rasmi kuanzia July 01 2021, kuanza kwa zoezi la Kitaifa la uhakiki wa umiliki wote wa ardhi kwa kutumia Kitambulisho cha NIDA kwa nchi nzima.
“Tunataka wamiliki wote hewa waliomilikishwa kimakosa, kiwizi, kiutapeli na kiujanja lazima tuwabaini lazima tujue kwa nini jina lako la kiwanja halifanani na majina ya hati yako ulipataje, hata kama una nyumba mbili hatukunyang’anyi hatuna ukomo wa umiliki” Waziri Lukuvi