Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ilala limesema hakuna madhara yaliyojitokeza kwa Binadamu kwenye tukio la Bar ya La Chaaz iliyopo maeneo ya Sinza, Dar es salaam kuungua moto na tayari moto umedhibitiwa kwa 80%.
“Hakuna madhara kwa Binadamu, kwa 80% moto umedhibitiwa, kabla hatujaja tuliwajulisha TANESCO, mpaka sasa hawajajua chanzo maana ndio wanazima moto hizi ni taarifa za awali tu”- Elinimo Shang’a Mkaguzi Msadizi wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji Ilala