Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus ni miongoni mwa watu waliotuma salamu za pole kufuatia kifo cha Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kilichotekea jana Jumatano Machi 17, 2021.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Ghebreyesus ameonyesha kuguswa na msiba huo mkubwa kwa Taifa la Tanzania na dunia kwa ujumla.
“Natuma salamu za pole kwa Serikali ya Tanznaia kufuatia kifo cha Rais John Magufuli tunaungana na familia na Taifa zima la Tanzania katika kuomboleza msiba huu na kuwafariji katika kipindi hiki kigumu” Tedros