Mtando wa kijamii wa Facebook umeizuia akaunti ya Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro kwa kueneza taarifa za uwongo kuhusu janga la corona (Covid-19).
Kulingana na Faebook, Maduro alikiuka sera za Facebook kwa kukuza utumiaji wa dawa inayoitwa Carvativir, ambayo inadaiwa kuwa nzuri na inafaa dhidi ya Covid-19.
Facebook, ambayo iliondoa video ya Maduro iliyokuwa ikitangaza dawa hiyo kwenye jukwaa lake, ilitangaza kufunga akaunti ya Rais wa Venezuela kwa siku 30.
Kwenye video hiyo iliyoondolewa na Facebook, Maduro alitaja dawa ya Carvativir iliyotengenezwa kwa mmea wa thyme kuwa kama “muujiza” na kudai kuwa inaweza kutumika katika kuzuia na kutibu virusi vya corona.
“JAFO KAMA UMESHINDWA TUAMBIE, TAMISEMI MNACHUKUA FEDHA HAZIRUDI”- RAIS SAMIA AWASHA MOTO