Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika ameibuka katika kijiji cha Oldadai wilayani Arumeru mkoani Arusha kwenye mazishi ya kijana Hance Remmy,nakudai ana uwezo wa kumfufua marehemu nakupelekea kushuka kwenye kaburi akiwa na ndugu wa marehemu kwa zaidi ya saa tatu bila mafanikio.
Kwa mujibu wa majirani waliozungumza na Ayo tv wamedai kwamba mtu huyo alianza mikasa hiyo kanisani lakini baadaye wakati wakuzika alionekana tena nakuzuia mwili huo kuzikwa nakushuka chini ya kaburi akiwa na ndugu wa marehemu lakini alishindwa kufanya hivyo nakutoka kwenye kaburi hilo nakukimbia ambapo baada ya tukio hilo ndugu waliamua kumzika kijana huyo majira ya usiku.