Mfalme Abdullah wa Jordan, na ndugu yake wa baba mmoja Mwanamfalme Hamzah leo hi wameonekana pamoja hadharani tangu kuzuka msuguano katika kasri la kifalme juma lililopita.
Kasri la kifalme limesambaza picha ya pamoja yenye kuwajumuisha Mfalme Abdullah, Mwanamfalme Hamza, Mwanamfalme Hussein na wajumbe wengine.
Picha hiyo imepigwa katika kaburi la Mfalme Talal mjini Amman, ambao ni mji mkuu wa Jordan.
Kwa Hamzah hii ndio mara yake ya kwanza kuonekana tangu alipowekwa katika kile kilichotajwa kizuizi cha nyumbani katika kipindi kilichogubikwa na tuhuma za kwamba anahusika na njama za kuuyumbisha ufalme wa Jordan.
Mfalme na mwanamfalme walikuwa katika tofauti ya nadra kutokea, ambapo Mfalme Abdulallah, alikuwa akikitazama kitendo hicho kama cha uchochezi ambacho kinamuhusisha ndugu yake huyo. Katika sakata hilo watu wengine 18 waliwekwa kizuizini.