Wakala wa zamani wa Neymar anayejulikana kwa jina la Wagner Ribeiro ameweka wazi kuwa Neymar alitakiwa na Real Madrid 2019 na walikuwa tayari kumsajili kwa euro milioni 300 (Tsh Bilioni 828) akitokea PSG ya Ufaransa.
Wagner anasema Rais wa PSG Nasser alikataa na kusema hata kwa euro Bilioni 1 (Tsh Trillion 2.7) Neymar hauzwi kwenda popote hivyo Real Madrid chini ya Rais wao Fiorentina Perez wakashindwa kufikia lengo lao.
“Wakati huo (2019) Neymar alikuwa anakaribia kujiunga na Real Madrid ambayo Rais wao Fiorentina (Perez) aliniambiwa wako tayari kulipa euro milioni 300 ila Nasser (Rais wa PSG) alikataa na kusema hata kwa euro Bilioni hauzwi”>>> Wagner VIA L’Equpe