“Katika mwaka 2020/2021 Serikali imechukua hatua za makusudi hususani utekelezaji wa miradi ya kielelezo, ujenzi wa viwanda, sambamba na kuimarisha sekta binafsi kwa ajili ya kuongeza fursa za ajira na ujuzi kwa Watanzania, hadi kufikia Februari, 2021 ajira 594,998 zimezalishwa katika Sekta mbalimbali, kati ya hizo, ajira 314,057 zimetokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ajira za Serikali na ajira 280,941 zimezalishwa kupitia Sekta binafsi”———Waziri Mkuu Majaliwa Bungeni Dodoma leo
“Kupitia Programu ya Kitaifa ya Kukuza Ujuzi Nchini, vijana 18,956 wamepatiwa ujuzi unaowawezesha kujiajiri au kuajiriwa, kati ya hao, Vijana 5,538 wamepatiwa mafunzo ya uanagenzi (Apprenticeship) katika fani za ufundi stadi ambapo Wanufaika 77 ni Watu wenye ulemavu”——— MAJALIWA
“Vijana 10,178 wamepewa mafunzo ya kurasimishiwa ujuzi walioupata kupitia mfumo usio rasmi wa mafunzo ambapo kati ya wanufaika hao 28 ni Watu wenye ulemavu, Vijana 3,240 wamewezeshwa kupata mafunzo ya uzoefu kazini (Internship) katika Taasisi binafsi na za umma ambapo kati yao wahitimu 92 ni Watu wenye ulemavu”———MAJALIWA
“Katika mwaka 2021/2022, Serikali itaendelea kuratibu utekelezaji wa masuala ya ukuzaji ajira na kazi za staha katika Sera, Mikakati na Mipango mbalimbali ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa ili kuhakikisha nguvu kazi ya Taifa inapata ujuzi stahiki pamoja na kuongeza fursa za ajira”——— MAJALIWA