“Serikali inaimarisha miundombinu ya usafiri wa anga ili kuchochea ukuaji wa Sekta nyingine za kiuchumi ikiwemo utalii, kilimo na madini, Miradi inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa Viwanja vya Ndege vya Geita ambao umefikia 98%, Songea 95% na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Mtwara ambao umefikia 53.2%”——— Waziri Mkuu Majaliwa Bungeni Dodoma leo
“Pia kuna maandalizi ya ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato utakaogharimu Tsh. Bilioni 759 yamekamilika, vilevile ujenzi na upanuzi wa Viwanja vya Ndege vya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Sumbawanga vitakavyogharimu Tsh. Bilioni 136.85 unaendelea”———MAJALIWA
“Sambamba na uimarishaji wa miundombinu ya usafiri wa anga, Serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa Ndege mpya tatu, mbili zikiwa ni Airbus A220-300 na moja ni Dash 8-Q400 De-Havilland, Ndege hizo zinatarajiwa kuwasili mwaka 2021/2022 na hivyo kuwezesha Serikali kuwa na jumla ya Ndege 12, nitumie fursa hii kulipongeza Shirika la Ndege Tanzania kwa kuanzisha safari za kwenda Guangzhou, China, Safari hizo, zitakuwa chachu ya kuimarisha biashara, utalii na ajira” ——— MAJALIWA