Kampuni ya Sahara Tanzania Limited imeongeza uwezo wake wa kuhifadhi bidhaa za Petroli hadi kufikia lita Milioni 27 katika nia ya kuongeza upatikanaji na uwezo wa ubora wa juu katika bidhaa za Tanzania na mataifa jirani ya Afrika.
“Tangu tuanze kazi Tanzania mwaka 2015, Kampuni ya Sahara imetanua miundombinu yake kutoka mashine 10 za kupakilia mizigo na matanki manne ambayo kwa pamoja yanahifadhi lita Milioni 36 hadi mashine 20 za kupakilia mizigo pamoja na matanki manane ambayo kwa pamoja yanahifadhi lita milioni 72 na kutanua maendeleo ya uchumi Tanzania kupitia upatikanaji bidhaa za Petroli,” amesema Meneja Mkazi wa Sahara Tanzania Limited, Olumuyiwa Aladejana.
Aidha, kampuni ina mpango mkakati wa kukuza uwezo wa upatikanaji na uhifadhi Automotivbe Gas Oil (AGO), Petrolium Motor Spirit (PMS) na JET A1. Mradi huo unataraji kuifanya Kampuni ya Sahara kuwa moja ya vituo vikubwa vya uhifadhi, kutoa nafasi ya kuongeza fursa za ajira na ukuaji uchumi wa Tanzania.
“Vilevile ni muhimu kutambua kuwa vituo vyetu vinajiendesha vyenyewe, pia tumedhamiria kujenga matanki mawili ya Liquefied Petrolium Gas ( LPG), ambayo itakuwa na uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 6,000 ikiwa ni sehemu ya kampuni kuendesha mapinduzi ya teknolojia na kuimarisha upatikanaji wa nishati safi kwa Tanzania, Rwanda, Zambia, Malawi na Congo,” Aladejana.
Aladejana wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya utendaji kazi wa Sahara Tanzania, aliweka wazi kuwa kampuni inafurahi kuona imepata fursa ya kuiunga mkono nchi katika mipango ya maendeleo ya mwaka 2025 kama kiongozi katika sekta ya mafuta na gesi, ambayo inachangia pakubwa ukuaji uchumi na maendeleo Tanzania.
Mipango ya maendeleo ya mwaka 2025 inaitangaza Tanzania kimataifa kwenye mipango ya maendeleo kama nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, ikiwa na viashiria vya maisha bora, amani, uimara, umoja na utawala bora pamoja na jamii iliyoelimika vema.
Vilevile, uchumi imara unawezesha kuimarisha ukuaji na faida jumuishi: “Sahara Tanzania ipo tayari kuchangia mafanikio ya mkakati huu mzuri kupitia shughuli zetu kwenye sekta ya nishati na kuingilia kati ikiwa ni moja ya miradi ya maendeleo Tanzania. Tunaipongeza serikali kwa sera imara na kusimama imara kuamini kuwa Tanzania ipo katika hatua ya kufanikisha mipango yake na Sahara itaendelea kuchangia pamoja na wadau wote kwenye hatua hii.”
Katika maelezo yake aladejana alisema inatia moyo kuona kampuni za nishati zinaungana. Sahara Group na kampuni kubwa za nishati barani Afrika zinaweka pamoja uimara wao katika soko la dunia la nishati.
Hata hivyo, amebainisha kuwa nchi za Kiafrika zinahitaji kuoanisha utambuzi wa bidhaa zao kukuza miamala kati ya Afrika.
“Tunaiona dunia inaegemea kwenye mafuta safi yenye kaboni kidogo na yenye salfa. Tukikuza bidhaa zetu utaongeza mtiririko wa bidhaa katika bara zima la Afrika na kanda zake, matokeo yake italifanya Bara la Afrika kuwa imara katika bniashara,” Aladejana.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Sahara Tanzania, Mwajabu Mrutu alisema kampuni hiyo imejitolea kuleta ukarimu nchini kupitia kuimarisha miradi yake ya huduma kwa jamii.
Alisema, mambo waliyoyafanya katika jamii ni pamoja na kuiongezea uwezo maktaba ya Shule ya Sekondari Pugu ambayo kwa sasa inahudumia wanafunzi 1000 pamoja na ukarabati wa vyoo katika Shule ya Sekondari Salma Kikwete ili kukuza Mipango ya Maendeleo Endelevu inayogusia usafi na usafi wa mazingira.
Aidha, kampuni imeendesha miradi ya uwezeshaji vijana, ikiwemo mwongozo wa kazi na ushauri binafsi wa masuala ya fedha pamoja na mkakati mkubwa wa MyFutureStarsWithMe ambao ulilenga kuwaonyesha vijana wa kitanzania kuwa hawatakiwi kukata tamaa katika ndoto zao.