Watoto 20 wamefariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea Shule moja katika Mji Mkuu wa Niger, Niamey. Imeelezwa, moto ulianza wakati watoto wakiwa kwenye vipindi na wengi wao walikuwa madarasa yaliyoezekwa kwa makuti.
Kwa mujibu wa taarifa, moto ulizuia lango la Shule na kupelekea Wanafunzi wengi kulazimika kujiokoa kwa kuruka ukuta. Wengi walioshindwa kufanya hivyo walikuwa Wanafunzi wa chekechea.
Chanzo cha moto huo ambao umeteketeza madarasa 28 yaliyoezekwa kwa makuti na kuharibu mengine 30 yaliyojengwa kwa matofali bado hakijafahamika.