Club ya Al Ahly Benghazi ya Libya itatuma malalamiko yake CAF na kuomba uchunguzi ufanyikea baada ya wachezaji wao watano na Kocha wao Msaidizi kupima na kukutwa na Corona.
Kabla ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates nchini Afrika Kusini na kupoteza 3-0, wachezaji hao walipmwa na kukutwa na Corona ila wakati wanapima kwa ajili ya kuondoka Afrika Kusini wote majibu yakatoka Negative wanaamini hujuma zilifanyika.
Hii imekuwa kawaida kwa timu wenyeji kutuhumiwa na timu mgeni kuwafanyi hujuma japo CAF bado hawajapata suluhu ya kubaini, Corona imekuwa ikidaiwa kutumiwa na watu wengi kama njia ya kudhoofisha timu mgeni.