Staa wa AC Milan raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic (39) anaweza kufungiwa miaka mitatu kucheza soka na faini ya Krona milioni 1 (Tsh milioni 273.6) kwa kosa la kumiliki kampuni ya betting (bethard) taarifa iliyotolewa na gazeti la Sweden la Aftonbladet.
Zlatan anadaiwa kumiliki asilimia 10 ya hisa za kampuni ya betting, CEO wa kampuni hiyo iliyosajiliwa Malta amethibitisha Zlatan kuwa mmiliki mwenza wa kampuni hiyo.
Kama FIFA na UEFA wakafanya uchunguzu na kuthibitisha hilo Zlatan Ibrahimovic atafungiwa miaka mitatu na faini sababu sheria za FIFA haziruhusu kwa mchezaji kushiriki betting au kuwa sehemu ya umiliki kwa kuondoa mambo ya kupanga matokeo.