Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amesema suala la uaminifu linahitaji kujadiliwa kutokana na vijana watanzania kulalamikiwa kutokuwa waaminifu kwenye miradi mbalimbali.
Spika Ndugai amesema hayo Bungeni mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kusem kuwa iko haja ya suala la uaminifu kujadiliwa na wabunge kwani kiwango cha uaminifu ni kidogo sana.
“Wawekezaji wengi wamekuwa wakilalamikia suala la uaminifu kwa vijana hasa vijana Tanzania uaminifu ni mdogo, katika miradi ndani ya sekta mbalimbali ukiwaweka unajikuta unafirisika eneo hili sijui dawa yake nini?,” Spika Ndugai
“Iko haja ya Viongozi wetu wa dini wa madhehebu mbalimbali kuweza kuhubiri kuhusiana na uaminifu, shuleni mitaala, na wazazi tujenge jamii ambayo ni ya watu waaminifu wasio kuwa na tamaa, leo ukiwekeza afu uje bungeni umewaachia miezi sita ujawatemebelea utakuta umepigwa” Ndugai