Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amewajia juu Wafanyabiashara waliopandisha bei ya mafuta ya kula wilayani humo na kutoa saa 24 kujitafakari kabla hajawachukulia hatua———“watafakari kabla sijazinguana nao”
Sabaya ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Kituo cha Mabasi Bomang’ombe wilayani Hai baada ya Wanachi kumlalamikia juu ya kupanda kwa bei ya mafuta ya kula kutoka Tsh Elfu 22 kwa Lita tano hadi kufikia Tsh. Elfu 35 katika kipindi cha mwezi mmoja.
Sabaya amesema hakuna tatizo la upungufu wa mafuta nchini isipokuwa wapo Wafanyabiashara wakubwa aliodai hawazidi watano waliokula njama na kukubaliana kupandisha bei ya mafuta ili kupata faida kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Sabaya ametoa saa 24 hadi kufikia kesho Jumatano April 21, 2021 saa 9 alasiri kwa Wafanyabishara kukabidhi nyaraka zenye bei waliyonunua mafuta hayo ili kujiridhisha na bei waliyonunulia na wasipofanya hivyo, atatangaza bei elekezi.