NI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu ambapo muda huu analihutubia Bunge na Taifa kutokea Makao Makuu Dodoma, unaweza ukatazama hapa Ayo TV & Millardayo.com inakupa mubashara kile kilichobora.
“Nimekuja kulihutubia Bunge baada ya Nchi yetu kupita kwenye kipindi kigumu, kama inavyokumbukwa March 17 Taifa letu lilipata msiba mkubwa wa kuondokewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Magufuli,hivyo tusimame kumuombea Mpendwa wetu”-Samia Suluhu
‘Mapenzi ya Watanzania kwa Hayati Magufuli yalidhihirika katika kipindi cha maombolezo ambapo wengi walijitokeza kumuaga, namshukuru Mungu kwa kutupitisha salama kwenye kipindi cha mabadiliko ya Uongozi, dhamana hii ni kubwa na yenye mitihani mingi”—Rais Samia
‘Niliwahi kusema na leo narudia tena kwamba Mimi na Hayati Magufuli ni kitu kimoja, kwahiyo mengi ambayo nimepanga kuyatekeleza ni yale ambayo yalielezwa na Hayati Magufuli wakati akilizindua Bunge hili”-Rais Samia
‘Tutarudisha imani ya Wawekezaji na kutoa vivutio kwa Wawekezaji, tunalalamikiwa sana, kumekuwa na mchakato mrefu Watu wanapotaka kuwekeza Tanzania, Serikali ya Awamu ya Sita tunakwenda kukomesha hili na Uwekezaji utakwenda kwa haraka”-Rais Samia