Wananchi Kata ya Vigwaza wawaomba watu wenye uwezo wa kifedha kuwasaidia mahitaji muhimu hasa chakula na mavazi baada ya mazao mengi kuharibiwa na maji mengi yanayotoka katika Mto Ruvu na kuharibu mazao yao huku wengine wakibaki wajane baada ya waume zao kufariki na kuwaachia majukumu ya kuendeza familia hali inayopelekea wale mlo mmoja kwa siku na hali ya kimaisha kuwa ngumu zaidi.
Mmoja ya wananchi waliongea na AyoTV, Esta Dotto amesema kuwa wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa chakula kutokana na mafuriko kuingia kwenye mashamba yao na hiyo inatokana na wao kuwa jirani na Mto Ruvu ambapo ukijaa maji yanaingia kwenye mashamba yao.
Kwa upande wake Maria Donati amesema yeye ni mjane na ana watoto sita hivyo suala la chakula kwake ni mtihani mkubwa na asipohangaika anakuwa kwenye wakati mgumu yeye na watoto wake ambao wanamtegemea yeye.
Kwa upande wa wafadhili walio wasaidia chakula wakina mama hao na wazee wanaishi kwenye kaya masikini shirika lisilokuwa la kiserikali la Who is The Hussain la Jijini Dar es Salaam limesema kuwa litaendelea kusaidiana na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kutoa misaada mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.
Mratibu wa shirika hilo Fatema Kermali wakati wakikabidhi vyakula kwa kaya maskini kwenye kata hiyo ambapo pia waligawa wilaya ya Mkuranga na kutumia kiasi cha shilingi milioni 52 kwa wananchi 600 ambapo kila wilaya wananchi 300.
“Tutaendelea kushirikiana na serikali kwa kufanya miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akisisitiza wadau mbalimbali kusaidiana na serikali ili kuwaondolea changamoto wananchi hasa wale ambao wanauhitaji kwenye huduma za kiafya elimu na masuala mbalimbali ya kijamii,” Kermali.