Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) amesema Demokrasia ni pamoja na kuheshimu Taasisi zinazounda Demokrasia ikiwemo Vyama vya Siasa.
Nape amesema “Sasa hivi kuna Wanachama wapo Bungeni wa CHADEMA lakini CHADEMA ilishawafukuza. Kwanini wapo Bungeni? Wanatakiwa wasiwepo. Tufuate Sheria”
Asema Mfumo wa Vyama vingi ulipokuja Katiba ilibadilishwa na Tume mbalimbali zilipendekeza namna ya kuendesha Vyama vingi ikiwemo Tume ya Jaji Nyalali.
Amesisitiza “Tumepitia Milima na mabonde kwenye Siasa hadi hapa tulipofikia. Wapo walioumia na Wengine kufurahi. Rais Samia katoa Uwanja wa Meza ya Mzungumzo. Kwakuwa yupo tayari kukaa meza moja, basi tusikatae mazungumzo”.
UJENZI DARAJA LA JPM KUKAMILIKA KABLA YA WAKATI, WEZESHI LAKAMILIKA 100%