Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amekiri kuwa Chama tawala kilishindwa kudhibiti rushwa wakati wa utawala wa Jacob Zuma.
Amesema chama cha African National Congress (ANC) kingefanya zaidi kuzuia rushwa, akitoa ushuhuda wake kabla ya uchunguzi wa kisheria kufanyika juu ya madai ya rushwa ya wakati wa utawala wa bwana Zuma.
Ramaphosa amesema ANC haikuwapa raia wa Afrika Kusini kile ambacho walikuwa wanakitarajia kwa kuwajibika , wakati rushwa ilidhoofisha utawala wa sheria.
“Wote tunakubaliana kuwa taasisi ingeweza kufanya jitihada zaidi kuzuia utumiaji mbaya wa madaraka na matumizi mabaya ya rasilimali ,” Ramaphosa
Rais Ramaphosa amezungumza kama Mkuu wa Tume ya ANC na anatarajia kuendelea kutoa ushahidi wake siku ya Alhamisi.
Mwanzo wa maelezo yake siku ya Jumatano, amesema ANC ingejaribu kutoa muangaza wa namna jambo hili lingechunguzwa ili wahusika wawajibike.