Katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Balozi wa Marekani, Donald Wright, amesema Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani inatoa fursa ya kuenzi nafasi na wajibu wa Vyombo hivi katika kuimarisha na kuhifadhi Jamii zilizo huru.
Pia, Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ni fursa ya kubainisha na kukumbusha kuhusu vitisho vinavyowakabili Waandishi na Taasisi za habari wakati zikitekeleza majukumu yao.
Balozi Wright amesema Waandishi wa Habari wanakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na mabadiliko ya Kiuchumi na Kiteknolojia yanayotikisa misingi ya Uandishi wa Habari, kuzuka kwa mitandao ya kueneza taarifa za uongo na Sheria kandamizi za Habari.
Asema “Janga la COVID-19 limeongeza uzito wa changamoto hizi lakini pamoja na vikwazo vyote hivi, nina matumaini kuwa bado kuna mustakabali mwema kwa Uhuru wa Tasnia ya Habari Nchini Tanzania”.