Mkurugenzi wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka amekifunga Kiwanda cha Fujian Hexingwang kwa kukosa mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
Uamuzi huo umetokana na vifo vya Wafanyakazi wawili wa Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Pwani baada ya kutokea mlipuko kwenye tanuru la kuyeyusha vyuma chakavu.
Dkt. Gwamaka amekitembelea Kiwanda leo Mei 5, 2021 na kubaini hakina mazingira mazuri kwa ajili ya usalama wa Wafanyakazi, jambo ambalo limesababisha vifo vya Watu waliokuwa kazini.
Miaka mitatu iliyopita NEMC ilikabiliana na Kiwanda hicho katika masuala ya uhifadhi wa mazingira na iliwahi kukifungia na kukipiga faini kwa nyakati tofauti.