Wanafuzi 27 waliokuwa wametekwa kutoka taasisi ya misitu katika Jimbo la Kaduna Kaskazini mwa Nigeria wameachiwa huru.
Walikuwa miongoni mwa wanafunzi 39 waliyotekwa kutoka katika vyumba vyao za malazi na genge la wahalifu waliokuwa wamejihami kwa silaha Machi, Mwaka huu.
Mamlaka zinasema wahasiriwa walioachiwa huru siku ya Jumatano watafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu baada ya kuzuiliwa kwa muda zaidi tangu visa vya utekaji dhidi ya wanafunzi kwa lengo la kuitisha kikombozi kuongezeka katika miezi ya hivi karibuni.
Kuachiwa huru kwa wanafunzi hao kunakuja siku moja baada ya familia zao kuandamana nje ya Bunge la Taifa hilo mjini Abuja kushinikiza mamlaka kuingilia kati suala hilo.
Nigeria imeshuhudia ongezeko la visa vya utekaji nyara wanafunzi tangu mwezi Disemba huku hali ya usalama ikiendelea kudorora maeneo tofauti nchini.