Mtoto wa Nabii maarufu nchini Nigeria Temitope Balogun Joshua maarufu kama TB Joshua,Serah Joshua amefunga ndoa na kijana wa kitanzania Brayani Moshi aliyekuwa anaishi Ungalimited Arusha katika parokia ya Moyo safi wa bikira Maria iliyopo Ungalimited
Padri aliyefungisha ndoa hiyo Festus Mangwangi amesema vijana hao walikutana masomoni Marekani na kwamba kijana huyo alikuwa anaishi Ungalimited
“Kule Nigeria ilikuwa ndoa ya kiserikali Kule Dubai walifunga ndoa ya kipentecoste maana huyu binti ni mpentekoste ndio maana wamekuja kufunga hapa ili Brayani aendelee kuwa mkatoliki”-Padri Mangwangi
Baba mdogo wa Brayani anayefahamika kwa jina la Victor amesema amefurahia kijana wao kufunga ndoa na binti huyo kutoka nchini Nigeria.