Siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuzungumzia kuibuka kwa matukio ya ujambazi na kuonya kwamba Wasipime Kina cha Maji, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro wanafatilia orodha ya muhalifu mmoja hadi mwingine.
IGP Sirro ameyasema hayo alipokutana na Maafisa wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ambapo amewapa mwezi mmoja kuhakikisha wanakomesha Vitendo vya Uhalifu.