Mbunge waJimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima akichangia mapendekezo katika muswada wa kamadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2021/2022 uliowasilishwa Bungeni na Waziri wake Dkt. Dorothy Gwajima leo May 11, 2021
“Leo nataka kuzungumzia chanjo za Corona, kuna chanjo ambayo imeruhusiwa kuanza kutumika inaitwa Jonson Jonson imeruhusiwa na Marekani watengeneza chanjo wenyewe wanasema madhara ya chanjo hii ni kushindwa kupumua sawasawa, kuvimba kwenye uso, mapigo ya moyo yanakwenda haraka na damu kuganda kama watengeneza chanjo wenyewe wanaonyesha kwenye website yao kuwa kuna shida hiyo basi sisi tuwe makini najua mheshimiwa Rais ameshaunda kamati lakini mimi kama Mbunge nina haja ya kujadili na ku-alert wawe makini wanapochagua aina ya chanjo hizi.” Askofu Gwajima
“kwa ujumla chanjo hizi zote zinaonyesha side effect kuganda damu, kushindwa kupumua na kifo sasa ni kweli tukikataa chanjo tunaweza kuzuiwa tusisafiri kwenda ulaya kwa sababu hatujajanchwa, tunakabiliwa na uchaguzi mbaya sana, tuchanjwe na kitu tusichokijua sawasawa au tusichanjwe tuzuiwe kwenda ulaya ninaomba sana wizara ya afya waangalie kwa makini sana kwenye suala la chanjo, wangalie madhara ya sasa, madhara ya siku zijazo na madhara ya Taifa”-Mbunge wa Kawe, Akofu Josephat Gwajima