Leo May 11, 2021 Kuelekea sikukuu ya Eid mashirika mbalimbali yameendeleza utaratibu kutoa zawadi za Eid hasa kwa watu wasiojiweza, leo Benki ya Exim imetoa msaada wa vyakula na vinywaji kwenye vituo vinne vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingiramagumu vya jijini Dar es Salaam, Mbeya, Shinyanga na Karatu ikilenga kuwawezesha watoto hao waweze kusherehekea vizuri sikukuu ya Eid El Fitr.
Msaadahuo ulikabidhiwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo wakiwa wameambatana nawafanyakazi wengine na ulihusisha mahitaji muhimu ikiwemo mchele, mafuta yakupikia, sukari, unga wa sembe, unga wa ngano, maharage pamoja na katoni zajuisi na maji ya kunywa.
JijiniDar es Salaam, akiwasilisha msaada huo katika kituo cha kulelea watoto yatimana wanaoishi katika mazingira magumu cha New Faraja Orphanage Centre kilichopo Mburahati jijini humo, MenejaMasoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu alisema imekuwa niutaratibu wa benki hiyo kusaidia makundi na taasisi mbalimbali kupitia ppangowake wa uwajibikaji kwa Jamii (CSR) unaofahamika kwa jina “Exim Cares”.
“Msaadahuu ni maalum kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, na ni mwendelezowa utaratibu wetu wa kile ambacho tumekuwa tukikifanya kila mwaka ambapowafanyakazi wa benki ya Exim pamoja na uongozi kwa ujumla tumekuwa tukiguswakuhakikisha kwamba watoto wanaoishi kwenye vituo hivi wanafurahia Sikukuu hizikama wenzao waliopo majumbani,” Kafu
Kafu alivitaja vituo vingine ambavyo vimekabidhiwa msaada huo ni pamoja naKituo cha Watoto Yatima cha Nuru kilichopo jijini Mbeya, Kituo cha ShinyangaSociety for Orphans na kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija vilivyopomkoani Shinyanga pamoja na Kituo cha Shalom Orphanage and Children Care Centre kilichopo wilayani Karatu.
ZaidiBw Kafu alitoa wito kwa watoto hao kuhakikisha wanasoma kwa bidii hukuwakitanguliza nidhamu kwenye kila jambo wanalofanya ikiwemo masomo na shughulizao za kila siku wawapo shuleni na kituoni hapo.
“Imekuwani furaha kwetu Benki ya Exim kuona kwamba tumekuwa tukipata wafanyakazi nawateja wenye mafanikio makubwa ambao baadhi yao wamepitia katika vituo hivi na kwasasawanafanya kazi zao kwa bidii na kwa weledi mkubwa. Ili hayo yatimie na kwenupia ni wajibu wenu kusoma kwa bidii pamoja na kutii maagizo ya walezi wenu kwanidhamu kubwa,’’ Kafu
Kwaupande wao wawakilishi wa vituo hivyo waliishukuru benki ya Exim kwa uamuziwake wa kuwakumbuka watoto yatima ili nao waweze kusherehekea vizuri siku kuuya Eid El Fitr kama ilivyo kwa familia nyingine majumbani huku wakiomba taasisihiyo na wadau wengine kuendelea kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbalizinazowakabili.
“Tunashukurusana benki ya Exim na wafanyakazi wote kwa kuguswa na kuona umuhimu wakuesherekea siku hii muhimu na watoto yatima. Tunaomba waendelee kuguswa iliwatusaidie zaidi katika kutatua changamoto nyingine ikiwemo suala la bima zaafya kwa watoto kwa kuwa baadhi yao hawana bima hizo muhimu.” Bi ZamdaIdrissa Mlezi Mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Faraja kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam.