Serikali ya Tanzania hivi karibuni inatarajia kuanza kutoa huduma ya upandikizaji wa mimba (IVF) kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22.
Hayo yamesemwa na Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima alipokuwa akiwasilisha bajeti kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2021/22.
Pia huduma za upandikizaji wa uboho (yaani rojorojo lililoko katika mifupa) ama bone marrow kwa Kiingereza kwa wagonjwa wenye saratani ya damu.
‘’Tutaendelea kutoa huduma zote za kibingwa kama vile upasuaji wa kutumia tundi dogo,upasuaji wa kichwa, shingo na koo, ‘’. Waziri Gwajima.
Huduma hiyo inaanza ikiwa ni miaka miwili sasa imepita tangu Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanza maandalizi ya utoaji wa huduma hiyo ikiwemo kusomesha wataalamu na kuandaa jengo litakalotumika kutolea huduma hiyo.
UTEUZI MPYA, RAIS SAMIA ATEUA WAPYA 21, DPP ATEULIWA JAJI, MAHAKAMA YA RUFANI NA KUU