May 15, 2021 kuna hiki kisa nakusogezea ambacho ni cha kusikitisha kidogo lakini kinafunzo pia ndani yake hasa kwa wanandoa, kisa kinaanzia hapa Lan Douglas ndio aliekuwa mpelelezi kwenye kesi ya mauaji ya Carol Park na aliipa kesi hii kwa jina la (Lady of the lake) “Mwanamke wa ziwani”. Agosti 12, 1997 yaligundulika mabaki ya mwili wa mwanamke kwenye Ziwa Caniston nchini Uingereza.
Upelelezi ulipofanyika kwa kina ulisadiki kuwa mwili huu ulikuwa wa Carol Park mwanamke aliepotea kwenye mazingira ya kutatanisha miaka 21 iliopita. Carol Park alikuwa ni mke wa ndoa wa Gordons Park.
Lan alicheza vizuri na taaluma yake ya upelelezi kwa muda wa miezi mitano mwisho kubaini kuwa Gordons ndio muhusika wa mauji hayo ya mke wake wa ndoa miongo kadhaa iliopita.
Sababu za Gordons kumuua Carol na kwenda kumficha chini ya ziwa kwa kumfunga na kitu kizito ni tabia mbaya ya Carol ya kuchepuka mara kwa mara.
Carol alikuwa na pepo la mchepuko hivyo kulala nje mwezi mmoja kwake ilikuwa ni kitu cha kawaida. Mbaya zaidi alikuwa na tabia ya “Wife- swapping parties”. Ambalo jambo hilo kwa jamii za kimagharibi ni kitu cha kawaida.
Wife swapping parents ni tabia ya mwanaume analala na mke wa rafiki yake na mwanamke nae analala na mume wa rafiki yake. Maamuzi ya Gordons yalikuwa ya kinyama japo Carol kweli alimtenda na kumfanyia uchafu mwingi usiokuwa na idadi.
Mwisho wa siku Gordons alifungwa maisha baada ya kukusanywa ushaidi vizuri na yeye mwenyewe kukiri kuwa kweli alimuua mkewe kwasababu alimkuta na mwanaume live.
“MNATUHARIBIA KAZI” WAZIRI MKUU ATINGA BANDARINI, AWABANA MADEREVA, ATOA MAAGIZO KWA MABOSS