Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amemsimamisha kazi kwa siku kumi Meneja wa TEHAMA na huduma za biashara wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Lonus Feruzi na Wasaidizi wake Frank Mushi na Idda Njau ili watoe maelezo kufuatia kuwepo kwa tatizo katika huduma ya manunuzi ya LUKU kupitia njia za kielektroniki na kusema endapo maelezo yao hayatojitosheleza wataondolewa kazini.
Kwa muda wa siku tatu, Wateja wa TANESCO wameshindwa kununua umeme wa LUKU kwa njia ya Kielekroniki hivyo kulilazimu Shirika hilo kuwaelekeza Wateja wake kununua umeme kwenye ofisi zake za Mikoa na Wilaya katika maeneo mbalimbali nchini.