Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini wakiongozwa na Kamishina Jenerali wa Zimamoto (CGF) John Masunga wametembelea makaburi ya waliofariki kwenye ajali ya moto Msamvu Manispaa ya Morogoro Agosti 10, 2019 .
Akizungumza akiwa Katika makaburi hayo ya Kola, Masunga amesema kila ifikapo Mei 4 ya kila mwaka Dunian inaadhimisha kilele cha Zimamoto na Uokoaji hivyo kwa hapa nchini sherehe hizo mwaka huu zimefanyika kuanzia Mei 17 hadi Mei 21 kutokana na changamoto mbalimbali ambapo kitaifa yamefanyika mjini Morogoro.
Amesema lengo la maadhimisho ya siku hiyo ni kuwakumbuka watu wote waliofariki kwa ajali ya moto hivyo wameona ni vyema wakatembelea makaburi hayo ili kufanya ibada maalumu kuwakumbuka marehemu hao.