Mtanzania Rawan Dakik leo asubuhi amefanikiwa kufika kilele cha Mlima Everest, ambao ndio mlima mrefu kuliko yote duniani (mita 8,850).
Kwa mujibu wa blog ya IMG, ambayo imeweka orodha ya watu waliopanda mlima huo ulio mpakani wa Nepal na China, Rawan ndiye mwanamke pekee wa Tanzania katika orodha hiyo.