Viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU) wamekubaliana kuwekwa vikwazo dhidi ya Belarus kufuatia tukio la Ndege kulazimishwa kutua ili kumkamata Mwandishi wa Habari aliye na mrengo wa Upinzani.
Roman Protasevich alikuwa kwenye ndege ikitokea Ugiriki kwenda Lithuania ambayo ililazimika kutua Mji Mkuu wa Belarus, Minsk ambapo alikamatwa.
Viongozi wa EU wamezuia Ndege za Taifa hilo katika anga la Ulaya. Pia, Mashirika ya Ndege ya Umoja huo yameelekezwa kutotumia anga la Belarus. Vikwazo zaidi vya Kiuchumi vinatarajiwa kuwekwa.