Wabunge wa Texas Marekani wamepitisha muswada utakaoruhusu Wakazi wa Jimbo hilo kubeba bunduki na kutembea nazo mtaani hata kama hawana vibali vya kubeba silaha tofauti na sasa ambapo sheria inataka yeyote anaebeba bunduki kuwa na leseni, awe pia na mafunzo ya kuitumia lakini pia historia yake lazima ichunguzwe.
Wanaounga mkono sheria hiyo mpya wanasema itaruhusu Raia wa Texas kujilinda wenyewe huko mitaani na huenda ikasaidia Raia kujibu mashambulizi pale Mtu mwenye silaha anapofyetua risasi bila sababu kwenye eneo la umma kama ambavyo imetokea Watu kuua Watu kanisani, super market na sehemu nyingine za umma.
Muswada huo ulipelekwa na Gavana Greg Abbott ambae ameahidi kuutia saini ili iwe sheria ambapo itakua ruhusa kwa Mtu yeyote mwenye miaka 21 na kuendelea kubeba Bunduki japo waliowahi kuwa na rekodi za uhalifu hawatoruhusiwa.