Azam FC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 34, Agrey Morris kwa penalti dakika ya 65 na Mzambia Obrey Chirwa dakika ya 81, wakati la Rhino limefungwa na Selemani Abdallah dakika ya 32.
Sasa Azam FC inasubiri mshindi wa mchezo kati ya mabingwa watetezi, Simba SC na Dodoma Jiji FC zinazomenyana usiku wa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa, DSM ikutane katika Nusu Fainali Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mwezi ujao.
Nusu Fainali nyingine ni kati ya Biashara United ya Mara na Yanga SC ya DSM itakayopigwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.