Jeshi la Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 11 waliokuwa wakisafirisha Dawa za Kulevya aina ya Heroine, Kg 20.24, katika eneo la Sangasanga mkoani Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya ACP Alhaj Kabaleke Salim Hassan amewaambia Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam kwamba Dawa hizo zilikamatwa katika gari yenye namba za usajili T21 DEA aina ya Toyota NOAH, ambayo watuhumiwa hao walikuwa wanaitumia kuzisafirisha kutoka mkoani Ruvuma kwenda Dsm na Tanga.
Kwa nyakati tofauti, mwishoni mwa April na Mei mwaka huu, Kitengo hicho cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kimewakamata watuhumiwa mbalimbali wa Dawa za Kulevya jijini Dsm wakiwemo raia wa kigeni wakisafirisha na kufanya biashara hiyo haramu.
Aidha, Alhaj ACP Kabaleke Salim Hassan amewatahadharisha wananchi hususani wale wenye nyumba ambao hupangisha wapangaji ambao hawajui wanafanya shughuli gani.