Serikali ya Tanzania na Bank ya maendeleo ya Afrika zimesaini mikataba miwili ya mkopo nafuu wa Dola za Marekani Milioni 140 sawa na shilingi Bilioni 333.39 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Malagarasi unaotarajia kuzalisha megawat 49.5.
Katibu Mkuu wizara ya Fedha na mipango Emmanuel Tutuba akizungumza katika hafla yautiaji saini uliyofanyika Jijini Dar es salaam ametoa mchanganuo wa fedha hizo kuwa Dola Milioni 120 zimetolewa na Bank ya Maendeleo ya Africa huku dola Milioni 20 zikitolewa na mfuko wa wa pamoja wa maendeleo ya watu wa China.
Aidha amesema kuwa mradi wa kufua umeme wa Malagarasi utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano ambapo kwa mwaka utazalisha wastani wa Megawati 181 ukitarajia kuhudumia wateja 4,250.
Utekelezaji wa mradio huo ambao pia Serikali ya Tanzania imechangia Dola za Marekani Milioni 4 .14 utakwenda sambamba na ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, shule za msingi mtambo wa kuzalisha umeme pamoja na kituo cha umeme.