Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetabiri hali ya upepo mkali kwenye maeneo mengi ya nchi katika kipindi cha msimu wa kipupwe, unaotarajiwa kuanza mwezi huu mpaka Agosti mwaka huu.
Akizungumzia utabiri huo leo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA ambaye pia ni Makamu wa tatu wa Rais katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dk Agnes Kijazi amesema msimu huu upepo utakuwa mkali kuliko ilivyo kawaida.
“Kwa kawaida msimu wa kipupwe hutawaliwa na upepo wa Kusi, lakini kutokana na matarajio ya uimarikaji wa wastani wa mgandamizo mkubwa wa hewa kusini mwa Afrika, vipindi vichache vya upepo mkali vinatarajiwa kujitokeza” Dk. Kijazi.