Rais Samia pia amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Wilayani Kinondoni ambapo pamoja na kupokea maelezo ya Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Zavery Peter Benela amewatembelea wagonjwa wanaopatiwa matibabu ya nje na waliolazwa wodini.
Rais Samia ametoa msaada wa shuka 200 kwa ajili ya wagonjwa na amewahakikishia wananchi kuwa Serikali itachukua hatua zaidi kutatua tatizo la upatikanaji wa dawa, kuboresha maslahi ya Madaktari na Wauguzi na kuboresha mazingira ya hospitali hiyo.
Rais Samia amewataka Watanzania wote kuendelea kuchukua tahadhari zinazoshauriwa na wataalamu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Korona (Covid-19).